Staa wa muziki wa kizazi kipya Bongo, anayemiliki jina la Ney wa
Mitego amenusurika 'kudanja' kufuatia mlipuko mkubwa wa moto wakati
alipokuwa akikamilisha zoezi la upigwaji picha (shooting) za video za
wimbo wake mpya uliopewa jina la Nasema nao ambao ndani ametoa diss
kibao kwa wasanii kadhaa wa muziki huo.
Akizungumza na media muda mfupi uliopita Ney ambaye sasa
amejipachika jina la 'True Boy'
amesema kuwa kulikuwa na matukio mengi
ya kushangaza wakati kuanza kwa zoezi la kuchukua video hiyo ikiwemo
watu kuungua moto na wengine kukatwa na mabati wakati wa harakati hizo
"Wakati tunaanza tu kuna mdogo wangu alikatwa na bati, halafu baada ya
muda tulishangaa mapipa yaliyokuwepo hapo yanalipuka moto mkubwa na
kumuunguza vibaya 'dairekta' wangu huku mimi nikinusurika baada ya
kuruka na kutua upande wa pili, mwanzoni hatukujua kama jamaa ameumia
sana lakini baada ya kumcheki siku iiyofuata tuligundua kuwa amebabuka
vibaya na ngoozi yote ya mkono imetoka kabisa" alisema Ney
No comments:
Post a Comment