Mb Dog.
Baada ya kupotea kwa muda mrefu kwenye ramani ya muziki, hatimaye Mb Dog
amevunja ukimya kwa kuachia wimbo mpya uitwao ‘The Only One’ alioufanya
kwenye studio yake mwenyewe aliyoifungua hivi karibuni, Makopa Inc.
Msanii huyo aliyetamba zamani na kibao ‘Latifa’ amesema kwa muda mrefu
alikuwa akifanya mambo yake nchini Ujerumani na sasa ameamua kurudi
kwenye game.
Mb Dog amesema hana
wasiwasi kuwa ataishika tena mioyo ya wapenzi wa muziki wa Tannzania
kwakuwa haoni kipingamizi na muziki haujabadilika sana.
“Navyoona najua muziki umechangamka katika njia zake, lakini sio kwamba watu wamebadilika kuimba na muziki utafanyika vile vile kama watu walivyozoea kuusikia, sema tu katika kuanzia kuna harakati zitakuwa tofauti muda mfupi wakati nikitulia kwasababu muda mrefu nilikuwa sijajihusisha na haya mazoezi kwasababu ya mambo yangu binafsi,” alisema.
Aliongeza kuwa ujio wake mpya unaweza kuwa zaidi ya Latifa, “hilo ni miongoni mwa mawazo niliyonayo kwasababu sijaona kama kuna vitu tofauti vinavyofanyika labda vya chinichini ambavyo sivifahamu, lakini kimuziki tu naona uko kawaida na ntafanya vizuri zaidi ya hata hivyo.”
Mb Dog amesema hajamsahau P-Funk Majani ambaye ndiye alimtambulisha kwenye muziki wa Tanzania kwa kumtengenezea hit ya Latifa. “Ujue yeye ndo kama father kwenye muziki huu, ni mtu ambaye akinifanyia kazi anatumia nguvu nyingi sana lakini sasa nimerudi, nimefanya hii ngoma mwenyewe sasabu yeye pia ana kazi nyingi, lakini kwasababu muda upo lazima niende pale kupiga ngoma mbili tatu watu waziskie kutoka pale. Katika albam yangu kuna watu muhimu kama yeye hawawezi kukosa kunipigia nyimbo.”

No comments:
Post a Comment