Lionel Messi.
Klabu ya Barcelona
imekiri kuwa kutokuwepo kwa mshambuliaji nyota wa kimataifa wa
Argentina, Lionel Messi katika mchezo wa kirafiki uliochezwa jijini
Humburg kwasababu ya maumivu umeikosesha klabu hiyo fedha nyingi. Barcelona
ilithibisha kuwa kukosekana kwa mchezaji huyo kucheza nchini Ujerumani
katika
mchezo wa Jumanne umeikosesha asilimia 30 ya mapato ambayo
ilikuwa ipate kutokana na mchezo huo ambayo inafikia kiasi cha dola
360,000. Katika
mchezo huo Barcelona ilifanikiwa kuifunga Humburg mabao 2-1 ambayo
yalifungwa na Dani Alves na Gerard Deulofeu ambapo timu hiyo pia
iliwakosa nyota wake wanaocheza katika timu ya taifa ya Hispania ambao
bado wako katika mapumziko baada ya kushinda taji la Ulaya nchini
Ukraine mapema mwezi huu. Barcelona
inatarajiwa kucheza mchezo mwingine wa kirafiki na timu ya Raja ya
Morocco Jumamosi lakini haijajulikana kama mchezaji huyo atakuwa amepona
kwa ajili ya mchezo huo.
No comments:
Post a Comment