Vincent Kompany.
Nahodha wa klabu ya
Manchester City, Vincent Kompany amesaini mkataba mpya wa miaka sita na
klabu hiyo ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu nchini Uingereza. Mchezaji
huyo wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye miaka 26 alijiunga na City
akitokea klabu ya Humburg ya Ujerumani mwaka 2008 na msimu uliopita
aliiwezesha klabu hiyo kushinda taji lake la kwanza la ligi toka kwa
1968. Kompany
alikaririwa katika tovuti ya klabu hiyo akisema kuwa ana furaha kuwepo
klabuni hapo hivyo hana sababu ya kuhangaika kutafuta mahali pa kwenda
ndio maana ameamua kusaini mkataba mrefu na klabu hiyo. Mchezaji
ambaye alianza kucheza katika klabu ya Anderletch ya nchini kwake kabla
ya kuhamia Ujerumani alinunuliwa na City wakati ikinolewa na Mark
Hughes ikiwa ni muda mfupi kabla ya Sheikhe Mansour kuinunua klabu hiyo
na kuanza kumwaga mahela katika kununua wachezaji nyota.
No comments:
Post a Comment