Idadi ya maiti za ajali ya kuzama kwa Meli ya MV Skagit
zimeongezeka na kufikia 89 baada ya miili mingine 11 kupatikana leo
katika maeneo manne tofauti ya visiwa vidogovidogo vilivypo mwambao wa
Zanzibar.
Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed
Mhina, amesema kuwa miili iliyopatikana leo, sita ni wanaume akiwemo
kijana mdogo na mingine mitatu ya wanawake.
Inspekta Mhina amesema, maiti zote zimezikwa katika makaburi ya
pamoja ya Kama yaliyopo nje kidogo ya mji wa Zanzibar chini ya usimamizi
wa Jeshi la la Wananchi wa Tanzanaia JWTZ, Jeshi la Polisi, MKMK, JKU
na Varantia.
Amesema miili hiyo ilipatikana katika viisiwa vya Pungume, Fumba,
Chumbe na eneo linalokupwa na kujaa maji la Funguyasini maeneo jirani
na kisiwa mama cha Unguja.
Naye Mkuu wa Polisi Kikosi cha Wanamaji na Bandari Zanzibar SP
Martin Lisu, amesema kuwa kunauwezekano mkubwa kuwa maiti hizo
zinaibuka kutoka katika meli hiyo ya Skagit.
Kamanda Lisu, amesema kuwa kutokana na kuendelea kuibuka kwa
maiti hizo, Maafisa wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wanaendelea na
zoezi lao la kutafuta miili mingine na kupokea taarifa za kuonekana kwa
mwili kutoka kwa watu wenye vyombo binafsi vya uvuvi na kuzifuatilia.
Hivi karibuni akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Jakaya Kikwete, Daktari Mkuu Mwelekezi wa Jeshi la Polisi
nchini Dk. Ahamed Makata, alisema kuwa maiti nyungi zitaweza kupatikana
ifikapo siku ya nne tangu kuzama kwa meli hiyo.
Alisema tabia ya maiti ya binadamu aliyekufa maji na kuzama,
haiwezi kukaa chini ya maji kwa muda mrefu kama haikufungwa na kitu
kizito kabla ya kuzama.
"Kwa kawaida maiti ya mtu aliyekufa maji haiwezi kukaa ndani ya
maji wakati wote na kwamba hata kama itaendelea kubaki majini lakini
katika muda wa kuanzia siku tatu na nne mwili ama miili hiyo nilazima
ianze kuibuka na kuelea juu ya maji". Alisema Dk. Makata.
No comments:
Post a Comment