John Mahama.
Baada ya kifo cha ghafla cha Rais John Atta Mills wa Ghana jana, saa chache baadae Makamu wa rais John Mahama ndio amekabidhiwa madaraka kwa sasa.
Kuhusu chanzo cha kifo cha Mills, BBC wamesema taarifa kutoka ofisi ya rais zinasema alifariki ghafla baada ya kupelekwa hospitali Jumatatu usiku na inaaminika aliugua ugonjwa wa kansa.

Kifo cha rais wa taifa hilo la pili duniani kwa ukuzaji wa cocoa kimekuja wakati alikuwa anajiandaa kugombea tena urais.
Rais Attah Mills ambaye husafiri mara kwa mara kwenda ng’ambo kwa matibabu alifariki muda mfupi baada ya kupelekwa hospitali Accra , Ghana ambapo ni siku chache tu zimepita toka apelekwe Marekani kwa uchunguzi wa kawaida wa afya yake.
Ghana ilikuwa inatarajiwa kwenda katika uchaguzi mkuu Disemba mwaka huu ambapo John Attah Mills alikuwa ametangaza nia yake ya kutetea hiyo nafasi, wakati wa uongozi wake, uchumi wa Ghana uliimarika na demokrasia kupanuka zaidi.
John Atta Mills ambae alianzisha uchimbaji wa mafuta nchini Ghana amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 68 na amefariki dunia siku tatu tu baada ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa July 21.

No comments:
Post a Comment