Thorgan Hazard.
Klabu ya soka ya Chelsea imefanikiwa kumnyakuwa mchezaji wa klabu ya lens ya Ufaransa, Thorgan Hazard ambaye ni mdogo wake Eden ambaye naye alisajiliwa katika kipindi hiki cha usajili kwa ada ambayo haijawekwa wazi. Thorgan ambaye ana umri wa miaka 19 amecheza mara 11 pekee katika Ligi Daraja la
Pili nchini Ufaransa inayojulikana kama Ligue 1akiwa na klabu ya Lens lakini pia amewahi kuziwakilisha timu za taifa za Ubelgiji za vijana chini ya umri wa miaka 16, 17, 18 na 19. Mchezaji huyo anatarajiwa kuanza mazoezi na timu ya Chelsea ya vijana chini ya miaka 21 kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi lakini suala la kumchukua mchezaji huyo kwa mkopo kutoka lens ndio linapewa kipaumbele. Kaka wa mchezaji huyo Eden alijunga na Chelsea June mwaka huu kwa ada ya paundi milioni 32 kutoka klabu ya Lille nayo ya Ufaransa.
Klabu ya soka ya Chelsea imefanikiwa kumnyakuwa mchezaji wa klabu ya lens ya Ufaransa, Thorgan Hazard ambaye ni mdogo wake Eden ambaye naye alisajiliwa katika kipindi hiki cha usajili kwa ada ambayo haijawekwa wazi. Thorgan ambaye ana umri wa miaka 19 amecheza mara 11 pekee katika Ligi Daraja la
No comments:
Post a Comment