Monday, July 23, 2012

DIWANI WA CCM AFA GAFLA: AANGUKA AKIWA KIKAONI.

Diwani wa Kata ya Mianzini iliyopo Mbagala Charambe jijini Dar es Salaam, Cesylia Macha, amefariki dunia ghafla wakati alipokuwa akizungumza na wajumbe wa kata hiyo
Diwani huyo alianguka juzi katika ofisi za CCM eneo la Kibonde Maji akwia katika mazungumzo na wajumbe wa kamati ya siasa wa kata hiyo na alikimbizwa Zahanati ya Zakhiem kupatiwa matibabu na alifariki akwia njiani kuelekea huko.

Imedaiwa diwani huyo alikuwa amesimama wakati alipokuwa akifanya mazungumzo hayo na kabla hajakaa kwenye kiti alianguka ghafla

Kifo hicho kimethibitishwa na Mwenyekiti wa kata hiyo Bw. Hakika na kusema walipomfikisha hospitalini hapo wakati wakiwa katika vipimo daktari alisema alishafariki dunia

Amesema maziko ya diwani huyo yanatarajiwa kufanyika leo saa 10 alasiri nyumbani kwake

Akitoa kwa kifupi historia ya marehemu alifafanua kuwa - Diwani huyo alijiunga na CCM mwaka 1977.

Mwaka 2000 aliamua kugombea ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Kata ya Charambe na ujumbe wa kamati ya siasa ya kata na kushinda nafasi zote hizo.

Mwaka 2005 aligombea udiwani wa Kata ya Charambe kupitia CCM na kuibuka mshindi

Mwaka 2010 aligombea udiwani kupitia CCM katika Kata ya Mianzini ambayo ilianzishwa baada ya kugawanywa kwa Kata ya Charambe ambako aliibuka kidedea

No comments: