na Akon, hakija kaa sawa P Square wakaongoza mfululizo kwenye habari za burudani Afrika baada ya kuachia kolabo yao na Rick Ross.
Upepo nauona kama unahamia Afrika Mashariki anytime soon, Ay ameshatangaza kolabo zale na Young Joc, Tyga na Tanto Metro and Devonte wa Jamaica, jipya lililonifanya nikupe hiyo intro, ni kuhusu mshkaji Mrwanda ambae wiki kadhaa zilizopita aliweka picha kwenye facebook akiwa kwenye party na mastaa wa dunia kama Ray J, baba yake Nick Cannon mume wa Maria Carey na mkali wa reggae Lady Dread.
Hizo line zinamuhusu Mwimbaji ambae ni mshindi mara mbili wa shindano la Tusker Project fame Alpha Rwirangira wa Rwanda ambae yuko Marekani sasa hivi akipiga kitabu cha muziki, amethibitisha kwamba single yake mpya inayokuja iitwayo I SWEAR imetengenezwa na mikono ya producer wa Hollywood Marekani KENNY CLOUDS ndani ya jumba la studio ya BLACK HOLE PRODUCTION.
Kinachotoa imani zaidi ya ukali wa hiyo single ni kwamba Huyo Producer nimekutajia tu lakini naona jina limekupita, lakini ni maarufu na mikono yake sasa hivi ndio inahusika kufanya mixing ya album mpya ya Snoop Dogg huyu huyu unaemsikia na kumuona.
No comments:
Post a Comment