Mrisho Ngassa.
Yanga wameendelea kuonyesha mabavu
katika usajili baada ya kumsajili Kelvin Yondani, Nizar Khalfan,
Barthez, Domayo na wengine wengi, leo taarifa za usajili kutoka klabu
hiyo zinasema kwamba klabu hiyo ipo kwenye mazungumzo na klabu ya Azam
ili kuweza kumsajili winga wa kimataifa wa Tanzania Mrisho Khalfan
Ngassa.
Habari za ndani zinadai kwamba Ngassa, Yanga na Azam wapo kwenye mazungumzo ya mwisho na huenda kutakuwa na habari nzuri kwa wapenzi wa Yanga juu ya kurudi kwa
kipenzi chao Ngassa mitaa ya Jangwani.
"Jana saa nne asubuhi Ngassa alifika pale makao makuu ya Yanga na akawa kwenye kikao kizito katibu wa Yanga na mmoja wa wadau wakubwa wa Yanga bwana Seif." - kilisema chanzo cha habari.
"Jana saa nne asubuhi Ngassa alifika pale makao makuu ya Yanga na akawa kwenye kikao kizito katibu wa Yanga na mmoja wa wadau wakubwa wa Yanga bwana Seif." - kilisema chanzo cha habari.
Katika usajili huo Yanga wapo tayari
kulipa kiasi kikubwa cha fedha na kumtoa kiungo Nurdin Bakary ili kuweza
kumtwaa winga huyo ambaye alishwahi kuichezea Yanga kwa mafanikio kalba
ya kuhama kwa uhamisho uliovunja rekodi ya ndani ya usajili baada ya
Azam kulipa milioni 60 kwa Yanga na kumtwaa Ngassa.

No comments:
Post a Comment