Siku ya Jumatatu, tarehe 18, June, 2012,
majira ya mchana, Katibu wa Baraza la Wazee wa klabu ya Yanga aliitisha
mkutano wa waandishi wa habari kwenye makao makuu ya klabu bingwa ya
Afrika Mashariki na Kati yaliyopo eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam.
Katika mkutano wake huo na waandishi wa habari jana Mzee Ibrahim Akilimali aliongelea mambo mengi yanayoihusu Yanga lakini pia aliniongelea mimi Shaffih Dauda. Akiwa na akili timamu na nina uhakika bila kulazimishwa na mtu, Mzee Akilimali alinitupia shutuma nzito ambazo nadiriki kuziita za uongo ambazo kwa kweli zinaweza au zimeshafanikiwa kuharibu jina langu kama mwandishi wa habari pia kama binadamu wa kawaida tu.
Hivyo kuniharibia sifa yangu nzuri ambayo nimejijengea kwa kutumia nguvu kuifanya vizuri kazi yangu. Mzee Akilimali alinukuliwa akisema kwamba mimi (Shaffih Dauda) nimekuwa ndio kikwazo cha ujio wa kocha wa kimataifa wa Brazil, Marcio Maximo kuja kuifundisha klabu ya Yanga. Aliendelea kusema kwamba mimi nimekuwa na mawasiliano na Maximo nikimwambia mambo mengi ya uongo kuhusu Yanga ili niweze kutimiza lengo langu la kumuona kocha huyo asije kuifundisha Yanga.
Alinukuliwa akisema kwamba nimekuwa nikimtumia ujumbe mfupi wa simu, barua pepe na kumpigia simu Marcio Maximo nikimwambia asije Yanga kwa kuwa timu hiyo ni maskini na wana madeni hivyo asijaribu kuja Yanga. Katibu huyo wa Baraza la Wazee la Yanga aliendelea kusema kwamba Maximo amewatumia ujumbe akiwaambia mimi namsumbua sana juu ya suala hilo hivyo sasa anaogopa mpaka kupokea simu za Tanzania kwa ajili ya usumbufu wangu Shaffih Dauda. Kiukweli hizi ni tuhuma nzito na chafu dhidi yangu, kamwe siwezi kukaa kimya na kuliacha hili lipite hivi hivi, hivyo nimeona bora nilitolee majibu.
Tuhuma za Mzee Akilimali sio tu zinaweza kunichafua bali pia zinanigombanisha na mamilioni ya wapenzi na wanachama ya klabu Yanga pamoja na wapenzi wote wenye kupenda maendeleo ya mchezo wa soka hapa nchini. Binafsi pamoja na wana sports xtra wenzangu tumekuwa mstari wa mbele kupigania maendeleo ya michezo hapa nchini hususani mchezo wa soka, ujio wa Marcio Maximo hapa nchini kuja kuifundisha Yanga naamini ungeweza kuisaidia klabu iyo pamoja na nchi kwa ujumla,sasa iweje nimzuie kuja nchini kufanya jambo la maendeleo kama hilo ?
Pia tuhuma hizi zinaweza kuniharibia kazi yangu kupitia vipindi vya michezo vya Sports Extra na Sports Bar ambavyo siku zote kwa pamoja na wenzangu tumekuwa tukifanya kazi ya kuhabarisha pamoja na kutoa mawazo yetu kuhakikisha soka na michezo kwa ujumla inapiga hatua kuelekea mbele. Mwisho baada ya kusema yote hayo nimefikia uamuzi wa kumpa siku saba (7) Mzee Akilimali kutoa ushahidi au vielelezo vya shutuma alizonitupia alivyodai anavyo ili kuweza kuthibitisha madai yake dhidi yangu,na kama akishindwa basi itabidi aitishe tena mkutano wa waandishi wa habari kama alivyofanya wakati akitoa tuhuma zake dhidi yangu na akanushe aliyoyasema na kuniomba radhi la sivyo sheria itachukua mkondo wake.

Huu ndo ushahidi wa alichokizungumza mzee wangu Akilimali.

No comments:
Post a Comment