According to globalgrind
ni kwamba juzi usiku glass zilizopasuliwa ziliharibu mazingira ya club
ya usiku ya WIP downtown Manhattan aka Manny-Hanny New York.
Drake, Meek Mill na Chris Brown walikua kwenye Club hiyo kwenye signing party ya Teyana Taylor kwenye label ya G.O.O.D MUSIC.
Mashuhuda wanasema Chanzo
cha huo ugomvi ni pale Chris Brown aliponunua chupa ya pombe na kumtuma
muhudumu ampelekee Drake, hapo ndipo rapper huyo Mcanada alipomaind na
kuamka.
Alimfata Chris Brown
alipokuepo na kuanza kulumbana kuhusu Rihanna na kupelekea kumpiga Chris
Brown usoni na kumchana mdomoni na chupa na kujihami kwa chochote
kitakachoweza kutokea.
Inasemekana Meek Mill ambae hapatani na CB anahusika kuchochea huo ugomvi manake ndio alikua pamoja na Drake.
Chris Brown muda mfupi
baadae alijipiga picha ya alipoumia na kuiweka kwenye page yake ya
twitter akiiambatanisha na kauli za matusi na kejeli, aliuliza chupa
kitu gani? kisha akaweka alama ya kicheko na kusema mchezo wa kurupigana
na chupa ni wakike, wanaume mnarusha chupa? kweli nyie dhaifu.

No comments:
Post a Comment