Kwa fans wote wa Big
Brother Africa najua kama ulipata chance ya kuchek show weekend
iliyopita najua sina haja ya kuuliza trending topic kwenye mitandao ya
kijamii ilimuhusu nani.
Ofcourse my girl Fetty the
best Dj Fetty wa XXL ya CLOUDS FM ndio alikua Dj aliepewa mwaliko wa
kuonyesha ujuzi jumamosi na jumapili.
Kwa show hizo mbili tu
alizopiga hakika Africa imemtambua ambapo tayari watu kadhaa wameweka
wazi nia ya kutaka kufanya nae kazi.
Fetty amesema baada ya show alifatwa na Channel O, kituo
cha Television cha South Africa chenye heshima kwenye burudani ambapo
kimetaka awe Dj kwenye show yao maarufu ya usiku ya Basement.
Fee’h amesema yuko nao
kwenye mazungumzo ambapo atatoa matokeo soon, vilevile amepata mialiko
ya nchi kadhaa za Africa kwa ajili ya kwenda kupiga kama Dj ambapo nchi
ya kwanza kumtumia maombi asubuhi yake baada ya kupiga show ni Rwanda,
bado hajawajibu mpaka sasa anavuta subira kidogo alafu afunguke…. kama
kutakua na any news… utakua wa kwanza kuifahamu kupitia johnsonvernon.blogspot.com!

No comments:
Post a Comment