Friday, June 22, 2012

DOGO JANJA ATUA DAR KWA PIPA

Dogo Janja.
Siku chache baada ya kuondolewa ndani ya kundi la Tip Tipo Connection, staa wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Abdul Abubakar Chende ‘Dogo Janja’ ametua Bongo Muda mfupi uliopita akitokea A-town (Arusha).
Taarifa ambazo zimeifikia kutoka pande za uwanja wa ndege wa JK Nyerere zinasomeka kuwa Dogo Janja ametua mida ya saa 4:30 kwa pipa (ndege) na kulakiwa na mashabiki wake waliojitokeza kwa wingi.
Akiwa jijini Arusha kabla ya kuanza safarai yake hii ya leo jana Dogo janja aliiposti kupita BBM maneno yaliyosomeka “Ki2 cha dua nini home lazima kieleweke” akimaanisha kuwa yuko kwenye kuomba dua ili safari yake ibarikiwe.

No comments: