
Beckham. 
Kiungo wa kimataifa wa 
Uingereza ametemwa katika kikosi cha nchi hiyo kitakachoshiriki michuano
 ya Olimpiki itakayofanyika jijini London mwaka huu. Beckham mwenye ana 
umri wa miaka 37 amewahi kuwa nahodha wa nchi kipindicha nyuma na 
alikuwa akitaka nafasi katika kikosi hicho kitakahoshiriki olimpiki 
kabla ya kuamua kutundika daluga. Akihojiwa mara baada ya kutangazwa kwa
 kikosi hicho Beckham 
amesema kuwa amesononeshwa na kuachwa kwake kwenye
 kikosi hicho lakini bado ataendelea kuwa mshabiki wa timu hiyo katika 
michuano hiyo na anaamini wataibuka kidedea na kunyakuwa medali ya 
dhahabu. Kocha wa kikosi hicho Stuart Pearce alimuingiza mchezaji huyo 
katika orodha ya wachezaji 35 lakini katika mchujo ili kubakia na kikosi
 cha mwisho cha wachezaji 18 kocha huyo alimchagua beki Micah Richards 
badala yake. Pearce alimpigia simu Beckham kumtaarifu hatomjuisha katika
 kikosi hicho kwakuwa alikuwa akihitaji kutengeneza kikosi ambacho 
kitakuwa cha kujihami zaidi katika michuano hiyo ndiyo maana akaamua 
kumchukua beki Manchester City Richards ili kusaidia kwenye suala la 
ulinzi. 
 
 
No comments:
Post a Comment