Jordi Alba.
Klabu ya Barcelona
imejipanga kujizatiti kwenye safu ya ulinzi msimu ujao baada ya
kufanikiwa kupata mbadala wa aliyekuwa beki wa klabu hiyo Eric Abidal
ambaye ni mgonjwa kwa kumsajili beki wa klabu ya Valencia Jordi Alba kwa
mkataba wa miaka mitano. Katika taarifa za klabu hiyo ambazo zimetumwa
katika mtandao wa kijamii wa twitter Alba mwenye miaka 23 ambaye kabla
ya kwenda Valencia alikulia katika
shule ya watoto ya Barcelona
amesajiliwa kwa ada ya euro milioni 14 baada ya kufaulu vipimo vya afya.
Barcelona imekuwa sokoni kwa kipindi kirefu ikijaribu kutafuta beki
ambaye ataziba pengo la Abidal ambaye amefanyiwa upasuaji wa kupandikiza
ini mapema mwaka huu na haijulikani kama beki huyo wa kimataifa wa
Ufaransa atarejea tena uwanjani baada ya kupona. Alba ambaye pia yuko
katika kikosi cha timu ya taifa ya Hispania alianza kuichezea nchi hiyo
Octoba mwaka jana ambapo aliitwa kuziba pengo la Joan Capdevila katika
mchezo dhidi ya Scotland na toka kipindi hicho hajaachwa kwenye kikosi
hicho.
No comments:
Post a Comment