Saturday, August 18, 2012

LIGI KUU ENGLAND YAANZA LEO; PREVIEW WIGAN NA CHELSEA HILI HAPA.

Eden Hazard
Eden Hazard.

     VIKOSI VYA LEO
WIGAN

Al-HabsiRamis, Caldwell, Figueroa
Boyce, McCarthy, McArthur, Beausejour
Miyaichi, Di Santo, Maloney
   
CHELSEA

CechIvanovic, Terry, Cahill, Cole
Mikel, Lampard
Ramires, Mata, HazardTorres


Pazia la Ligi Kuu ya England linafunguliwa leo. Mabingwa wa Ulaya, Chelsea wanakuwa vigogo wa kwanza kushuka uwanjani, wakimenyana na Wigan ambayo inaingia kwenye msimu mpya ikiwa bado na Roberto Martinez, ambaye ilibaki kidogo tu atimkie Aston Villa na Liverpool zilizokuwa zinasaka makocha wapya.
Baada ya kumnasa winga Mjapani, Ryo Miyaichi kwa mkopo wa muda mrefu kutoka Arsenal, safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo imeongezewa makali na Arouna Kone aliyetua kutoka Levante katikati ya wiki, wakijiandaa kwa maisha mapya bila Hugo Rodallega. Victor Moses anaweza kuondoka pia wakati wowote, akijiunga na moja kati ya klabu hizo mbili.
Kama ilivyo kwa wenyeji wao, Chelsea inaanza msimu mpya bila majeruhi wa kutisha, wakati Branislav Ivanovic atacheza licha ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Manchester City, kwani haihesabiki.
Klabu hiyo itatakiwa kuangalia hali ya mshambuliaji wake, Daniel Sturridge, ambaye alitemwa kwenye kikosi cha England kilichomenyana na Italia kwa sababu ya majeruhi, lakini kuna uwezekano akawa fiti kucheza japo kidogo, wakati Marko Marin ana maumivu ya nyama.

     JE WAJUA?
    Wigan ilimudu kufunga mabao 42 msimu uliopita, machache zaidi ya Bolton (46) iliyoshuka daraja na Blackburn (48).

    Kikosi cha Roberto Martinez kinafungua dimba la Ligi Kuu kama msimu uliopita walipotoka sare ya 1-1, bao la kusawazisha la dakika za lala salama la Jordi Gomez's likiwanusuru kufungwa, baada ya Daniel Sturridge kutangulia kufunga.

    Mfungaji bora wa klabu hiyo msimu uliopita alikuwa mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Franco Di Santo, ambaye alifunga mabao saba.

    Victor Moses (pichani kulia) anaweza kukamilisha uhamisho wa kuhamia Stamford Bridge kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

    Chelsea imetumia pauni Milioni 65 kwa usajili wa wachezaji kama Eden Hazard, Oscar na Marko Marin.

    Klabu hiyo imeshindwa kufunga katika mechi nane tofauti msimu uliopita, wakati Wigan ilikuwa mechi 12.

    Frank Lampard na Juan Mata kwa pamoja wamefunga na kutoa pasi 35 za mabao katika mechi 63 za ligi msimu uliopia baina yao.

    Walimaliza msimu wakiwa hawajaruhusu bao hata moja kwenye mechi 10, saba chini ya mabingwa Manchester City

No comments: