Saturday, August 18, 2012

WACHINA NOMA, WATENGENEZA HADI SAINI FEKI YA MARADONA.

Diego Maradona - Al Wasl
 Diego Maradona.
 Gwiji wa soka Argentina, Diego Maradona (pichani) ameingia kwenye zengwe lingine, la kufojiwa kwa saini yake na msaidizi wake wa zamani. Maradona anaelezwa kujiandaa kushitaki kampuni mbili za China, Sina na The 9 Limited, baada ya kutumia picha na jina lake kwenye soka yao 'Hot Blooded Soccer' bila ridhaa yake, . Ilidhaniwa saini ni ya mwenyewe kocha huyo wa zamani wa Argentina, lakini Maradona amesema hajawahi kusaini makubaliano hayo.  

No comments: