NANI KAISAHAU HII?
Kocha wa Manchester City, Roberto Mancini amesema jirani zake, United wana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England - kwa sababu wana washambuliaji wawili wakali mno.
Mashetani Wekundu wamemnunua Robin van Persie kutoka Arsenal kwa pauni Milioni 24 na watamtumia kwa pamoja na Wayne Rooney pale mbele

"Van Persie alikuwa mshambuliaji bora msimu uliopita," alisema Mancini. "Na Rooney, watakuwa pacha moja ya hatari sana katika Ligi Kuu.
"Nilikuwa siriaz wiki iliyopita wakati ninasema Manchester United walikuwa wana nafasi kubwa."
City ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu 'kizali zali' katika siku ya mwisho ya msimu - ikifunga mabao mawili katika dakika ya mwisho dhidi ya QPR na kuipiku United katika mbio za taji kwa tofauti ya mabao.
Ilikuwa mara ya kwanza wanatwaa ubingwa wa Ligi Kuu baada ya miaka 44, dhidi ya United, ambayo imechukua taji hilo mara 11 tangu kuanzishwa kwa mfumo wa Ligi Kuu mwaka 1992.
Na Mancini anaamini historia na uzoefu vinampa Sir Alex Ferguson nafasi kubwa ya kurejesha taji Old Trafford..

TOP SIX ZILIVYOSAJILI:
- Manchester City: Jack Rodwell £12m
- Manchester United: Robin van Persie £24m, Shinji Kagawa £12m, Nick Powell £3m
- Arsenal: Olivier Giroud £13m*, Santi Cazorla £12m*, Lukas Podolski £11m*
- Tottenham: Gylfi Sigurdsson £8m*, Jan Vertonghen £8m*
- Newcastle: Gael Bigirimana undisclosed, Romain Amalfitano free, Curtis Good undisclosed, Vurnon Anita £6.7m*
- Chelsea: Eden Hazard £32m*, Oscar £25m, Marko Marin £7m*, Thorgan Hazard £1m*
* reported fee
No comments:
Post a Comment