Manji kulia, akiwa amechuchumamaa kumsalimu Bi Rukia, mwanachama maarufu wa Yanga.
Wakati kamati
ya uchaguzi ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) inatarajiwa kuketi
Julai 2 kwa ajili ya kupitia pingamizi zilizowasilishwa kwa wagombea
uongozi wa klabu ya Yanga, wagombea wawili Yusuf Manji na Stanley Yono
Kevela wamewekewa pingamizi.
Klabu ya Yanga inatarajiwa kufanya uchaguzi mdogo julai 15 jijini Dar
es Salaam ili kuziba nafasi za baadhi ya viongozi waliojiuzulu akiwemo
mwenyekiti Lloyd Nchunga.
Mjumbe
wa kamati hiyo iliyo chini ya mwenyekiti wake Deogratius Lyatto, Salum
Mbwezeleni alisema kwamba kamati yake itapitia pingamizi hizo kwa
kusikiliza wapingaji na waliopingwa na kisha kutoa maamuzi.
Hata hivyo,
Mbwezeleni hakuweza kutoa ufafanuzi wa pingamizi wa wagombea hao Manji
(Uenyekiti) na Kevela (Makamu Mwenyekiti, Ujumbe) kwa madai kuwa bado
hajapitia maelezo yaliyowasilishwa na waliopinga.
“Ninachoweza
kusema kwa sasa ni kuwa kamati itakutana Julai 2 na kuwasikiliza
wahusika wote na kisha tutatoa maamuzi ili majina yaweze kutangazwa na
wagombea waanze kampeni zao,”alisema.
Kamati ya
uchaguzi ya Yanga chini ya mwenyekiti wake Jaji Mstaafu John Mkwawa wiki
iliyopita ilitawataja waliopitishwa katika ujumbe ni pamoja na Jumanne
Mwamenywa,Edgar Fongo, Beda Tindwa, Ramadhan Said,Omary A. Ndula, Shaban
Katwila,Ramadhan Y. Kampira,Lameck Nyambaya na Peter H. Haule.
Wengine ni
Justine S. Baruti,Abdalah A. Mbaraka, Kevela,Mosess K. Valentino,Aaron
Nyanda,George M. Manyama.Abdalah Sharia Ameir,Jamal Kisongo na Gaudiusus
Ishengoma.
Huku wanaowania
nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Ayoub Nyenze, Kevela na Clement A.
Sanga, wakati Jonh Paul Jambele, Manji, Edgar W. Chibula na Sarah
Ramadhan wameomba katika nafasi ya uenyekiti,”alisema.
Uchaguzi
huo ambao umepangwa kufanyika Julai 15 mwaka huu, umelenga kuziba
nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wanne wa kamati ya
Utendaji ambao walijiunzulu.
No comments:
Post a Comment