Thursday, June 28, 2012

AUNT EZEKIEL KAHAMIA DAR.

 
Staa wa filamu nchini Tanzania, Aunty Ezekiel hayupo nchini kwa muda mrefu sasa na habari zinasema amepiga kambi Dubai, huko.
 
Uarabuni ambako anaendesha maisha yake ya kila siku.Kutoweka kwa msanii huyo kulijulikana wiki iliyopita kwenye uzinduzi wa filamu ya Wema Sepetu ya Super Star pale Hyatt Kilimanjaro Kempinsk Hotel, Dar es Salaam ambapo wadau wengi walihoji aliko msanii huyo kutokana na tabia yake ya kutokosa shughuli.
Baadhi ya marafiki zake walisema yuko Dubai akiendesha maisha yake baada ya kuchoka na skendo za Bongo.
“Mnamuulizamuuliza Aunty, hamjui yupo Dubai, amechoka na maskendo ya Bongo, sasa anakula raha tu,” alisema shoga yake mmoja ambaye si maarufu, lakini hakauki kwenye viwanja vya kujirusha.
 
Habari nyingine zinasema Aunty atarejea nchini wiki mbili zijazo lakini hatakaa sana atarudi tena Dubai kuendelea na maisha yake ambayo si ya kucheza filamu tena kama ilivyokuwa hapa Tanzania.
 

No comments: