Prezzo akishukuru kabla ya kuondoka uwanja wa ndege.
Mwakilishi
wa Kenya katika shoo ya Big brother StarGame 2012, msanii Prezzo
amewasili jijini Nairobi (Kenya) jana asubuhi na kufuta minong’ono
iliyokuwa imezagaa nchini humo kuwa ana bifu na aliyekuwa mshiriki
mwenzake katika shindano hilo Alex Malonza.
Akiongea baada ya kuwasili jijini Nairobi jana Prezzo alisema hadhani
kama ana kinyongo na aliyekuwa mshiriki mwenzake. Tunamnukuu “I held no
grudges with Malonza, even though he nominated me twice”. Akimaanisha
hana kinyongo na Malonza ingawaje alimpigia kura ya kutaka awe mmoja wa
wanaotakiwa kutoka mara mbili.
Akiendelea prezzo alisema nimesikia anataka kufanya kazi za kisanii na
mimi, sidhani kama nina tatizo na hilo kwani sina kinyongo nae. Mimi
nipo kwa ajili ya chochote ambacho kitafanya mkono uende kinywani kwa
hivyo tusubiri na kuona matokeo ya kile kinachofikirika ama
kitakachowezekana.
akijibu swali la kama bado anampenda mshiriki mwenzake toka Nigeria
Prezzo alijibu tumeongea na tutakutana Nairobi siku si nyingi nafikiri
bado kuna nafasi ya kujadiliana kwa mapana zaidi.
Prezzo ameshika nafasi ya pili katika shindano la mwaka huu na kupata
nafasi ya kuteuliwa kuwa balozi wa kampeni ya kupiga vita njaa “One
Campaign” na pia amepata nafasi ya kwenda nchini Marekani baadae
mwishoni mwa mwezi huu kushuhudia shoo ya rapa nguli wa hip hop Jay Z
jijini New York.
Kuwasili kwa prezzo jana asubuhi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Jomo Kenyatta kulipelekea shughuli kusimama katika uwanja huo kwani watu
wengi waliacha shughuli zao na kwenda kumlaki huku wakimpongeza kwa
kufika hatua ya fainali na kukosa ushindi kidogo na wengine wakimpa
mkono pamoja na kumkumbatia na kupiga naye picha. Prezzo anatarajiwa
kukutana na Makamu wa Rais wa Kenya Mheshimiwa Kalonzo Musyoka muda
wowote leo au kesho
Prezzo akitoa ishara ya pamoja.
Prezzo akiwa na mama yake ndani ya gari lililompeleka nyumbani.
No comments:
Post a Comment