
Wakilishi wa Afrika
katika soka kwenye michuano ya Olimpiki inayoendelea jijini London timu
za Misri na Senegal zimefanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo
baada ya kutinga hatua ya robo fainali. Misri waliingia katika hatua
baada ya kuichapa bila ya huruma timu ya Belarus kwa mabao 3-1 na
kutinga hatua hiyo ambapo sasa watakutana na timu ya Japan katika mchezo
utakaochezwa Juamosi katika Uwanja wa
Old Traford jijini Manchester.
Senegal nao walitinga hatua hiyo baada ya kutoa sare ya bao 1-1 dhidi ya
Umoja wa Falme za Kiarabu-UAE bao ambalo lilisawazishwa na mshambuliaji
nyota wa timu hiyo Moussa Konate ambapo mpaka sasa amefunga mabao manne
katika michuano hiyo. Nchi hiyo sasa itapambana na Mexico ambao
wanaongoza kundi B baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya
Switzerland huku wenyeji wa michuano hiyo Uingereza wenyewe watacheza na
Korea Kusini. Timu inayopewa nafasi kubwa ya kunyakuwa medali ya
dhahabu kwa mara kwanza katika michuano hiyo Brazil wenyewe watamenyana
na Honduras katika robo fainali ya michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment