Tetesi za J'pili magazeti Ulaya


MAN CITY NA MAN UNITED KATIKA VITA KUWANIA SAINI YA KINDA LA EVERTON

Manchester City iko tayari kuanza mpango wa kumsajili mchezaji wa Everton, Jack Rodwell, lakini Manchester United na Chelsea nazo pia zinamtolea macho kinda huyo wa umri wa miaka 21.
Roberto di Matteo amepuuza tetesi kwamba Daniel Sturridge, mwenye umri wa miaka 22, anaweza kuondoka Chelsea.
Jack Rodwell
Roberto Mancini anavutiwa na Jack Rodwell, lakini atapata ushindani kuipata saini yake
Arsenal inampigia hesabu kiungo wa Malaga, Isco, na klabu hiyo ya Hispania inayokabiliwa na matatizo ya kifedha inataka ada ya pauni Milioni 8 kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka  20.
Mpango wa Stoke City kumsajili Michael Owen unaonekana kama kushindikana hivi, baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32, mshambuliaji wa zamani wa England, kutoridhia vipengele  vya mkataba.
Manchester United na Chelsea zimemkosa Muargentina Lucas Ocampos, mwenye umri wa miaka 18, ambaye sasa atajiunga na AS Monaco akitokea River Plate.
Liverpool bado ina nia ya kumsajili Theo Walcott, na kocha Brendan Rodgers anamuhitaji sana kuimarisha kikosi chake.
QPR inamtaka beki mzoefu, William Gallas, ambaye ameambiwa anaweza kuondoka Spurs.
Kocha wa Swansea City, Michael Laudrop amesema klabu yake haiwezi kuhofia kununua wachezaji chipukizi wa Kiingereza japokuwa wanauzwa bei mbaya.

KHALDOON AL MUBARAK

Mwenyekiti wa Manchester City, Khaldoon Al Mubarak anataka mazungumzo ya amani baina ya kocha Roberto Mancini bosi wa Utawala wa FA, Brian Marwood baada ya waili hao kutofautiana juu ya sera ya usajili.
Andre Villas-Boas anajiandaa kumpa mikoba kinda wa umri wa miaka 19, mshambuliaji Harry Kane katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu, baada ya kushindwa kuwaingiza Emmanuel Adebayor na Leandro Damiao.
Kocha Blackburn, Steve Kean yuko chini ya shinikizokuelekea mwanzoni mwa msimu, baada ya Shebby Singh, Mshauri wa wamiliki wa timu hiyo, kusema atafukuzwa iwapo Rovers itapoteza mechi zake tatu za mwanzoni.
Carlos Tevez amewavutia makocha wa Manchester City, baada ya kurejea mazoezini kwa moto mkali tofauti na msimu uliopita.