Van Persie.
Meneja wa klabu ya
Manchester United, Sir Alex Ferguson amewashambulia Arsenal kuhusiana na
nia yake ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Uholanzi
anayecheza katika klabu hiyo Robin van Persie. Ferguson anawalalamikia
Arsenal kwa kumuweka gizani toka alipotangaza ofa yake ya kumnunua
mshambuliaji huyo katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi. Akihojiwa
kuhusiana na suala hilo Ferguson amesema kuwa ni vigumu kugundua kwanini
wanafanya hivyo kwani wamejitahidi kadri ya uwezo wao lakini hakuna
kinachoendelea mpaka sasa. United walikuwa wamemtengea Van Persie kitita
cha paundi milioni 15 lakini Arsenal Arsenal wenyewe wanataka kumuuza
mchezaji huyo kwa paundi zaidi ya milioni 20.
No comments:
Post a Comment