Tetesi za Ijumaa magazeti Ulaya
LUCA MODRIC ALAZIMISHWA SPURS
Luka Modric amelazimishwa kufanya mazozi kivyake katika Uwanja wa mazoezi wa Tottenham, lakini Real Madrid inaweza kuachana kabisa na mpango wa kumsajili kiungo huyo wa Croatia mwenye umri wa miaka 26.
Chelsea imehamishia ndoana zake kwa nyota wa Napoli, Edinson Cavani, mwenye umri wa miaka 25, baada ya kuzidiwa na Zenit St Petersburg kwa mshambuliaji mwenye umri wa miaka 26 kutoka Porto, Hulk.
Joe Allen aliishuhudia Liverpool ikifungwa katika mechi ya Europa League na FC Gomel akiwa kwenye eneo la Wakurugenzi wa klabu hiyo ya Anfield, kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22 akiwa mbioni kusaini klabu hiyo kwa pauni Milioni 15, akitokea Swansea City.
Kiungo wa kimataifa wa Uholanzi, Wesley Sneidjer ameitaka Inter Milan kumnunua mchezaji mwenzake wa Uholanzi, mwenye umri wa miaka 27-, beki Nigel de Jong, kutoka Manchester City.
Chelsea inampigia hesabu beki wa kulia wa Juventus, Stephan Lichtsteiner, mwenye umri wa miaka 28, baada ya mpango wao wa kumsajili beki wa Hispania mwenye umri wa miaka 22, Cesar Azpilicueta wa Marseilles kuzimika.
Middlesbrough ina matumaini ya kukamilisha uhamisho wa mkopo wa kiungo wa Chelsea mwenye umri wa miaka 19, Josh McEachran.
Kiungo wa Celtic, Ki Sung-Yeung, mwenye umri wa miaka 23, sasa anawaniwa na Atletico Madrid pamoja na Arsenal.
Mchezaji wa Chelsea, Romelu Lukaku, mwenye umri wa miaka 19, anatakiwa kwa mkopo na West Brom, baada ya wakala wa mshambuliaji huyo, Christophe Henrotay kupiga chini dili na Fulham.
Mshambuliaji wa Caen, M'Baye Niang, mwenye umri wa miaka 17, anaweza akazistaajabisha Arsenal, Manchester City na Tottenham kwa kujiunga na AC Milan kwa mkopo.
OTHER GOSSIP
Beki wa Chelsea, John Terry, mwenye umri wa miaka 31, anaweza kuachwa kwenye kikosi cha England kitakachocheza mechi ya kirafiki dhidi ya Italia kutokana na kocha Roy Hodgson kutarajiwa kufanya mabadiliko kikosini.
No comments:
Post a Comment