
Andy Carroll.
Mshambuliaji wa klabu ya
Liverpool Andy Carroll ameitwa katika kikosi cha timu hiyo ambacho
kitacheza mchezo wa kufuzu kwa ajili ya michuano ya Kombe la Ligi ya
Ulaya maarufu kama Europa League dhidi ya timu ya FC Gomel kesho ingawa
hatma yake bado haijajulikana. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa
Uingereza kushiriki kwake kwenye mchezo huo utakaochezwa chini Belarus
hautaathiri uwezekano wake wa kutumiwa katika mashindano mengine.
Hatahivyo klabu ya West Ham bado wana matumaini ya kupata saini ya
Carroll ingwa wamekiri kimya kimya kwamba wanaweza kushindw mbio hizo
baada ya Newcastle nao kuingia katika kinyang’anyiro hicho. Sheria za
Shirikisho la Soka Duniani-UEFA linaruhusu mchezaji kucheza mchezo wa
kufuzu michuano ya Europa League na baadae kuhamia klabu nyingine
kucheza michezo ya hatua makundi.
No comments:
Post a Comment