QUEEN DARLIN AMSUPPORT DIAMOND KUHUSU MSIMAMO DHIDI YA BABA YAO.
- Diamond na dada yake wakiimba pamoja kwenye show ya Diamonds Are Forever.
Dada yake na mwanamuziki wa Bongo Flava aliyefanikiwa sana Diamond
Platnumz, Queen Darlin ameibuka na kumuunga mkono kaka yake huyo kwa
kutojali maneno ya baba yao kuwa hawamjali.
Kupitia magazeti ya udaku wiki iliyopita baba yake mzazi na Diamond alidai kuwa mwanae Diamond amemtenga na wala hamjali.
Alidai kuwa hamsaidii kama anavyofanya kwa mama yake na pia simu zake hazipokei.
Queen
Darlin naye amesema baba yao huyo alimtosa pia kipindi alipokuwa mdogo
kiasi cha kushindwa hata kuwafahamu baba zake wadogo.
Akihojiwa na
Clouds Fm, Diamond alielezea sababu ya yeye kumpotezea baba yake ni
kutokana na kumtelekeza na hivyo kulelewa na mama yake zaidi.
“Inamaana
ananijua mimi mwanae baada ya kujua mimi nimekua Diamond, siku zote
kama alijua mimi ni mtoto wake basi angekaa angenisomesha angenipa elimu
nzuri, lakini siku zote nilihangaika na mama yangu mzazi na ndo maana
siku zote mama yangu mzazi kipaumbele.
“Nisingependa kusikia mtu
yoyote anadiriki kuzungumza kwamba mimi ndo baba yake, wasitake
kuonekana kipindi cha maslahi mtu ndo anajifanya yeye ndo anahusika sana
na mimi kama mtoto wake, sipendi.”
Mi nimeanza kusema tangu natoa
wimbo wa binadamu, nasema upendo popote, ulipo kwa baba yangu (anaimba)
japo alinikataa, katika wimbo wa binadamu hata sijui kama leo ntakuja
kuwa na Prado. Hata kabla ya kuwa hivi niliimba before kabisa, sina
mbele sina nyuma, ina maana nisionekane na thamani mtoto wa fulani sasa
hivi, kwasababu nimekuwa fulani, hapana wasinitengenezae mazingira mbaya
mbele ya wananchi.
Mzazi wangu ataendelea kuwa baba yangu tu,
lakini asifikiri kupata priority kama anayopata mama yangu kwasababu
angetaka hiyo angeonesha kunijali na kunithanimi mapema kama mzazi.”
- Diamond na mama yake.
- Diamond, mama yake na dada yake.
- Mtu na dada yake.
No comments:
Post a Comment