Mshambuliaji wa kimataifa
wa Brazil na klabu ya Santos, Neymar amedokeza kuwa anampa nafasi
mshambuliaji nyota wa Barcelona kunyakuwa tuzo ya mchezaji bora wa dunia
inayojulikana kama Ballon d’Or kwa mwaka huu. Messi
ambaye ni raia wa Argentina anapewa nafasi kubwa ya kunyakuwa tuzo hiyo
baada ya kuonyesha kiwango cha juu katika timu yake na kuiwezesha
kunyakuwa mataji manne katika msimu wa mwaka 2011-2012 huku akiwa
amefunga mabao 73 katika mashindano yote. Akihojiwa
baada ya wadau kumfananisha na Messi, Neymar alipingana na kauli hizo
akisisitiza kuwa anategemea nyota huyo wa barcelona kushinda tuzo hiyo
kwani hakuna mchezaji wa aina yake kwenye soka hivi sasa. Messi
ambaye anaongoza kwa kufunga mabao mengi katika historia ya Barcelona,
alimfikia Michel Platini ambaye kwasasa ni rais wa Shirikisho la Soka la
Ulaya-UEFA kwa kunyakuwa tuzo ya Ballon d’Or mara tatu mfululizo.
No comments:
Post a Comment