Tuesday, July 24, 2012

MOURINHO KUKABIDHIWA TUZO NCHINI KWAO.


 Jose Mourinho.
Kocha wa klabu ya Real Madrid, Jose Mourinho anatarajiwa kutunukiwa tuzo inayojulikana kama Fernando Soromenho Prestige inayotolewa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini Ureno-CNID kutokana na mafanikio yake katika soka. Mourinho mwenye umri wa miaka 49 atapokea tuzo hiyo katika hoteli ya Pstana Palace iliyopo jijini Lisbon baada ya kuzungumza na vyombo vya habari. Tuzo hiyo ni

mojawapo ya tuzo za juu kabisa zinazotolewa na CNID ambayo ilianzishwa mwaka 1967. Mourinho ambaye alianza kazi ya ukocha katika klabu ya Benfica mwaka 2000 alikiongoza kikosi cha timu ya Porto kushinda taji ya Kombe la Ulaya na Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya katika kipindi cha miaka miwili ambayo amekuwa akiifundisha klabu hiyo. Baada ya kuondoka Porto alienda kuifundisha Chelsea ya Uingereza na Inter Milan ya Italia kabla ya kujiunga na Real Madrid mwaka 2010 ambapo ameiwezesha klabu hiyo kushinda Kombe la Mfalme mara moja pamoja na taji la Ligi Kuu nchini Hispania inayojulikana kama La Liga.

No comments: