
Meneja
Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando akizungumza na Waandishi
wa Habari, wakati wa uzinduzi wa namba fupi *150*60# itakayotumika
kupata orodha
(Menu)
ya Airtel Money pamoja na kuzindua promosheni inayomuwezesha mteja wa
Airtel kutuma na kupokea pesa bure. Kulia ni Afisa Uhusiano wa Airtel
Tanzania, Jane Matinde. Uzinduzi wa promosheni na utambulisho wa namba
hiyo fupi ulifanyika katika makao makuu ya Airtel mjini Dar es Salaam
jana.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania, imeendelea
kuboresha huduma ya Airtel Money kwa kurahisisha upatikanaji wa mwongozo (menu)
kwa kupiga **150*60# Bure, pamoja na kuzindua promosheni kabambe itakayowawezesha
wateja wa Airtel nchi nzima kutuma pesa bure.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Meneja
Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando alisema;” “Airtel tunaendelea kutoa uhuru
kwa wateja kupata
huduma zetu, kwa urahisi zaidi nchini kote, kuanzia sasa
mteja akipiga **150*60#, anapelekwa moja kwa moja kwenye orodha yake ya huduma
na kuweza kuchagua
anachohitaji kufanya, ikiwa ni pamoja na kuongeza salio,
kufanya malipo,
kutoa pesa na mengine mengi, alisema: “Tumefanya hivi, ili kumwezesha mteja mwenye simu yeyote
kupata huduma za
kibenki na kuondoa changamoto zozote zitakazojitokeza, sasa
mteja ana uhuru wa kuchagua kutumia njia ya awali, ambayo ni kwenda moja kwa
moja kwenye mwongozo wa simu yake na kupata orodha (Menu) ya Airtel au
kupiga namba *150*60# na kuunganishwa moja kwa moja,”alisema.
“Vile vile tunayo furaha kuzindua ofa kabambe kwa wateja
wetu nchini zima, ambapo kutuma au kupokea pesa chini ya kiwango cha 100, 000
ni BURE na mteja atakaponunua LUKU kupitia Airtel Money ni BURE (hakuna
viwango vya miamala vitakavyotozwa).
Tunawajulisha wateja wetu wote na wakala
wetu waliosambaa nchi zima kutumia huduma hii iliyo rahisi ni rahisi,”
aliongeza Mmbando.
Airtel Tanzania ni mtandao ulioenea nchini na unatoa huduma
za kifedha za Airtel Money yenye mawakala zaidi ya 10,000 waliosambaa maeneo
mbalimbali mjini na vijijini kwa dhamira ya kupunguza changamoto ya upatikanaji
wa huduma za kifedha na kusaidia wateja wetu kuokoa muda kwenda mbali
kupata huduma za kibenki.
Kupitia Airtel Money, mteja anaweza kupata huduma mbalimbali
ikiwemo: kupokea pesa, kulipa bill kama DSTV, LUKU na DAWASCO, USA
visa , kununua salio na huduma nyingine nyingi.
No comments:
Post a Comment