Akizungumza muda mfupi uliopita Baghdad amefunguka kuwa ameshangazwa
na hatua za wasanii hao kuchukia na kuamua kumtishia maisha kufuatia
'interview' yake na Gossip Cop wa XXL huku wakijua kuwa
alichokisema
kilikuwa ni ukweli kwa lengo lengo la kuwafungua watu kuhusiana na
matatizo wanayokumbana nayo wasanii wanapokuwa kwenye kazi zao
“Labda wataniteka wakiwa rumande, kwani
nimeshalifikisha suala hili polisi na tayari wamepewa saa 48 kuripoti”
kituoni alisema Baghdad.
Baghdad kilinuka upande wake kufuatia
stori iliyovujisha kwenye interview hiyo kuwa wasanii Mabeste, Suma
Mnazareti,Tash na Mensen Selecta walilala mchongoma (chumba kimoja)
kufuatia promota aliyewapeleka pande hizo kusepa bila kuwapa mkwanja
waliokuwa wamekubariana na hali kuwa mbaya upande wao.
No comments:
Post a Comment