Wanafunzi watano wameteketea kwa kuungua kwa moto
nchini Uganda baada ya moto kuunguza mabweni mawili ya Leos Junior Academy
katika manispaa ya Masaka.
Wanafunzi wote waliofariki ni wa elimu ya msingi
ambao wameungua hadi kutotambulika, na miili yao imepelekwa katika hospitali ya
rufaa ya Masaka.
Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Kusini Simon Peter
Wafana amesema tayari polisi nchini humo imeanzisha uchunguzi wa chanzo cha moto
huo.
Hii ni mara ya pili moto kuzuka katika shule hiyo
katika kipindi cha miaka miwili.
No comments:
Post a Comment