j
Asamoah Gyan.
Mshambuliaji wa
kimataifa wa Ghana na klabu ya Sunderland, Asamoah Gyan anatarajiwa
kusaini mkataba wa kudumu wa miaka mitano na klabu ya Al Ain ya Falme za
Kiarabu-UAE ambako alikuwa akicheza kwa mkopo ambapo atakua akilipwa
paundi 140,000 kwa wiki na klabu hiyo. Kwa mujibu wa taarifa
zilizotolewa na gazeti moja la michezo nchini Ghana klabu ya Sunderland
itavuna kiasi cha paundi milioni 21 kutoka kwa Al Ain kwa kumnyakuwa
mshambuliaji huyo moja kwa moja ambaye mkataba wake wa mkopo ulikuwa
unamalizika msimu huu. Mkataba huo mnono utakuwa umeipa faida kubwa
Sunderland ambao walinyakuwa mshambuliaji kutoka klabu ya Rennes ya
Ufaransa kwa ada ya paundi milioni 13 baada ya kung’aa katika michuano
ya Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini akiwa na kikosi cha
timu ya taifa ya Ghana. Baada ya kutua Sunderland aliwashtusha wadau
soka pale alipokubali klabu hiyo kumtoa kwa mkopo kwenda klabu ya Al Ain
kwa ada ya paundi milioni 6 Septemba mwaka 2011 ambapo akiwa huko
alifanikiwa kushinda mabao 27 katika michezo 24 liyocheza na kuiwezesha
klabu hiyo kunyakuwa ubingwa wa Ligi Kuu ya huko ambayo inafahamika kama
Pro League.
No comments:
Post a Comment