Malkia wa Bongo Move, Rose Ndauka yu taabani kitandani akisumbuliwa na ugonjwa wa Maralia.
Habari zenye ukweli asilia 100 ambazo ni kuwa Rose alianza kushambuliwa na ugonjwa huo siku ya jumatano asubuhi kulazimika kukimbizwa katika Zahanati iliyopo Magomeni Mikumi jijini Dar.
“Ni kweli nasuburiwana maralia, lakini hata hivyo leo nashukuru mungu ‘dizain’ kama nimepata nafuu na nimeweza kuzungumza na wewe’ alisema Rose akijibu swali kutoka kwa mwandishi aliyemtilia maguu hospitalini hapo huku akiwa ameshikiria mrija wa drip iliyokuwa ikining’ia juu ya kitanda chake.
Hata hivyo wakati taarifa hii inaruka hewani taarifa mpya imefika kwenye meza ya duara kuwa Rose amepewa ruhusa ya kurejea ‘home’ sambamba na ushauri wa kupiga msosi kiasi cha kutosha ili apete nguvu
........Stori by Dismas Ten…....
No comments:
Post a Comment