Basi la
kampuni ya Ngorika limepata ajari jana 25/6/2012 majira ya asubuhi pale maeneo ya kwa mrefu
Mkoani Arusha wakati likianza safari kuja dar es salaam likiwa na abiria 54.
Ajali hiyo imetokea wakati dereva akiwa kwenye mwendo wa kawaida tu ambapo
ghafla kwenye eneo wanapopaita kibao cha njano kabla ya mteremko wa daraja la
Nduluma dereva alishangaa kuona gari jingine likiwa limetokea mbele yake bila ya
kujua limetokea wapi na alipojaribu kulikwepa
ndipo basi
lilipopoteza welekeo na kupinduka, Lakini hakuna abiria
aliyeripotiwa kufariki bali abiria wengi walilipotiwa kujeruhiwa kwenye ajali
hiyo.
No comments:
Post a Comment