Mzee Majuto( Kushoto) akiwa na Sharo milionea
Nguli wa sanaa ya vichekesho Bongo, Amri Majuto ‘Mzee
Majuto’ amesema anakaribia kuachana na fani hiyo iliyomletea
umaarufu na heshima kubwa kote nchini.
Katika mahojiano ya dakika 20 aliyofanya na mtandao huu
akiwa wilayani Bagamoyo Mzee Majuto alisema kuwa anataka kufanya kazi
zake mwenyewe sambamba na vijana wachache aliowachagua kuepuka
dhuluma anayokutana nayo kutoka kwa wajanja wanaotajirika kupitia
migogo yao huku wakitoa malipo kiduchu kwa wasanii.
“Binafsi nalipwa Laki tano mpaka sita kwa filamu moja ambayo
nina uhakika mtengezaji anakwenda kuingiza zaidi ya milioni
themanini, sasa kuna haja gani mimi kuendelea kufanya kazi hizo”,
alihoji Mzee Majuto.
Akiendela zaidi mchekeshaji huyo mwenye heshima kipee kwa
wapenzi wa filamu nchini alisem akuwa si kama anaacha kuigiza moja
kwa moja lakini atahamia katika kufanya kazi zake binafi tofauti na
hizi za watu ili aweze kunufaika na jasho lake .
Hivi ninavokwambia tayari nimeshanunua baadhi ya vifaa vya kazi
na baadhi nategemea kuvipata ifikapo mwezi wa 9 mwaka huu , alisema
Majuto na kuongeza kuwa hakika nitageukia kwenye kufanya kazi zangu
mwenyewe ili na mimi nifaidi jasho langu” alimaliza mchekeshaji
huyo.

No comments:
Post a Comment