Monday, June 25, 2012

MWANADADA TOKA KENYA APATA SHAVU LA KUIGIZA NA STAR WA HOLLYWOOD 'BRAD PITT' NA WENGINEO.


Lupita Nyo’ngo.
Kama umewahi kuiona series ya Shuga inayotengenezwa na MTV bila shaka ulishaiona sura ya mwanadada huyu mrembo mwenye ngozi nyeusi na nga’aavu kama bati lililoakisi mwanga wa jua, Lupita Nyo’ngo ana kila sifa ya kuwakilisha uzuri wa msichana asili wa kiafrikaa.

Brad Pitt.
Baada ya kufanya vizuri kwenye show hii ya ‘Shuga‘, mrembo huyo amekula shavu la kushiriki kwenye movie ya Steve McQueen iitwayo ‘12 Years A Slave‘.
Kwenye movie hiyo atakutana na waigizaji ‘heavy weight’ wa Hollywood akiwemo Brad Pitt, Alfre Woodard, Chiwetel Ejiofor, Michael Fassbender, Ruth Negga, Adepero Oduye, Paul Dano, Benedict Cumberbatch, Scoot McNairy, Garret Dillahunt, Paul Giamatti na Sarah Paulson.

No comments: