Kijana mmoja anayedaiwa kuwa Mkristo 'Mlokole' na aliyejitambulisha
kwa jina moja la Joseph, jana mjini Morogoro alidhihirisha madai hayo
baada ya kumvamia jamaa mmoja aitwaye Magari Ramadhani ambaye ni muumini
mzuri wa dini ya Kiislam na kumwambia kwamba alikuwa ametumwa kumfanyia
maombi.
Hayo yalifanyika katika Uwanja wa Jamhuri mjini hapa ambapo alimtaka
muumini huyo kuvua barghashia ili apate nafasi ya kumshika kichwani.
Ramadhani alikubali ombi hilo na Joseph akamfanyia maombi, jambo
lililowafanya watu waliokuwa jirani kuangua vicheko.
Hata hivyo, habari zilizopatikana baadaye zilidai kwamba kijana huyo
ana upugufu wa akili, na Ramadhani naye alipohojiwa alisema anamfahamu
kijana huyo kwamba ni mgonjwa wa akili hivyo aliamua kumridhisha na
kumpa nafasi ya kumfanyia kile alichoita maombi.
No comments:
Post a Comment