Monday, June 25, 2012

KUMBE DIAMOND PLATNUMZ ALING'ANG'ANIWA NA TRAFFIC JUZ IJUMAA AKIWA KWENYE MISELE.



 Diamond Platnumz.
 
Naseeb Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ amejikuta aking’ang’aniwa kiaina na polisi baada ya kumbamba akiendesha mkoko wake mpya ambao haujasajiliwa.

Tukio hilo lililotokea ijumaa Juni 22, mwaka huu maeneo ya Bamaga jijini Dar ambapo Diamond aliangukia mikononi mwa maafande hao ambao walimbananisha kwa kosa la kuendesha gari lake jipya ambalo halijasajiliwa, aina ya Toyota Land Cruiser Prado.

Diamond alipowaonesha kadi halali na vibali vingine vya (TRA) walimwachia na kumtaka akaweke namba halali.

No comments: