
Kamanda Kova .
 Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova 
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la utekaji nyara na 
kujeruhi lililompata kiongozi mgomo wa Madaktari Steven Ulimboka 
anayedaiwa kutekwa na watu watano wakati akipata kinywaji katika klabu 
ya Leaders Kiondoni jijini Dar es salaam.

 Waandishi wa habari waimsikilza kamanda Suleiman Kova katika kituo kikuu cha polisi Kati jijini Dar es salaam leo mchana.
Kamanda Kova amesema Ulimboka aliokotwa na msamaria mwema ambaye 
hakutaka kumtaja jina lake kiusalama na kutoharibu upelelezo kuwa 
msamaria mwema huyo alimuokota Ulimboka katika msitu wa Mabwepande na 
kutoa taarifa kituo cha polisi cha Bunju, ambapo polisi aliyekuwa zamu 
alichukua maelezo yake na baadae Steven Ulimboka kuletwa katika 
hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
 
 
Dk Steven 
Ulimboka akiwa amejruhiwa vibaya na watu wasiojulikana baada ya kutekwa 
na kupigwa vibaya usiku wa kuamkia leo na kuokotwa huko Mabwepande. 
Kamanda Kova amesema jeshi la Polisi Kanda Maalum limeunda jopo maalum 
kwa ajili ya uchunguzi na upelelezi wa tukio hilo la utekaji nyara, 
kwani ni tukio la kwanza kutoke nchini, ameongeza kwamba wahusika wote 
watakaobainika kuhusika na tukio hilo wachukuliwa hatua za kisheria na 
sheria itafuata mkondo wake ili kukomesha matukio mengine kama hayo.
 
 
No comments:
Post a Comment