Mwanamuziki Koffi Olomide alitambulisha jumba lake
kwenye sherehe ya ufunguzi wa jumba hilo ambalo limegharimu mamilioni ya
shilingi na kunakshiwa kwa samani za bei ghali.
Mashabiki walipokea kwa hisia tofauti kitendo cha
Mwanamuziki Koffi Olomide kuweka wazi Jumba lake la
kifahari huku
wengine wakimpongeza na wengine wakimwambia kitendo hicho ni kama
dhihaka kwa wacongoman ambao wengi wao wanaishi kwenye dhiki kali huku
weingine wakiwa wanataabika kupata mlo wao lakini wanajitolea kuchanga
kununua kazi zake au kuingia kwa show zake.
Kiukweli ni jumba la kifahari sana na alialika watu mashahuri kwenye sherehe hii ambayo ilitumia pesa nyingi.
Jumba hili limejengwa kwenye vilima vya Fleury
almaarufu kama a mont-fleury eneo maarufu kama Msaki ambapo watu wenye
pesa ndio wanaishi huko. Koffi ni mmoja wa wanamuziki wakubwa si tu kwa
Congo bali Afrika nzima ambaye kiukweli amekuwa na mafanikio makubwa
tangu aanze muziki na amejizolea mashabiki wengi kote Ulimwenguni
kutokana na muziki wake.
No comments:
Post a Comment