John Mnyika.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema), Mhe. John Mnyika
ametolewa
nje ya bunge muda huu na Naibu Spika, Job Ndugai baada ya kukataa
kufuta kauli yake kuwa Rais Kikwete ni dhaifu wakati alipotakiwa kufanya
hivyo. Mnyika ametolewa nje ya bunge wakati wabunge wakichangia mjadala
wa bajeti ya serikali mwaka wa fedha 2012/13 iliyowasilishwa bungeni
hivi karibuni. Mnyika atarudi bungeni kesho.
No comments:
Post a Comment