MWANAMUZIKI
wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo Staili’, Hassan Musa ‘Super
Nyamwela’ amevunja ukimya na kuamua kubeba jumla msichana alimpachika
mimba aitwaye Hawa Maulid.
Super Nyamwela
alifunga ndoa Jumapili iliyopita kwenye Msikiti wa Kinondoni-Studio,
Dar es Salaam na
kufuatiwa na sherehe ‘hevi’ iliyofanyika nyumbani kwa
Hawa maeneo hayo ya Kinondoni na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo
mastaa wenzake.Baada ya ndoa, jioni ya siku hiyo pati nyingine ya kukata na shoka iliendelea kwenye Ukumbi wa Meeda Sinza jijini Dar ambapo wageni waalikwa walipata nafasi ya kuserebuka huku wakila na kunywa na kuwatuza maharusi.
Super Nyamwela alisema anamshukuru
Mungu kwa kumpatia mke mwema kwa mara nyingine baada ya kukaa muda
mrefu kutokana na mke wa kwanza kufariki na kumuachia watoto wawili.
No comments:
Post a Comment