KUFUATIA mafanikio alinayoyapata hivi sasa
kwenye anga ya muziki wa kizazi kipya Bongo, staa wa muziki huo Naseeb
Abdul ‘Diamond’ ndiye mkali aneingiza mkwanja mrefu zaidi kuliko nyota
wote wanaotamba hivi sasa hapa nchini.
Uchunguzi
uliofanywa na Teentz.com umebaini kuwa Diamond anaingiza kiasi cha
shilingi za kibongo Milioni 16 kwa kila shoo mbili anazofanya akiwa
ndani na nje ya jiji la Bongo.
Katika
kuhakikisha kuwa ukweli unapatikana Teentz ilimsaka Diamond na baada ya
kufanikiwa kumpata alikiri kufikia kiwango hicho .
“Nashukuru
Mungu kwa kufika hapa na ukweli ni kuwa nalipwa mkwanja huo na hii
imekuja kufuatia kuweka nguvu zangu katika muziki na kufanya vitu vizuri
kwa kuwa gemu ndiyo maisha yangu” alisema Diamond.
Akiendelea zaidi nyota huyo wa ‘Songi’
la ‘Mawazo’ alianika kuwa mafanikko haya yanakuja pia kutokana na
sapoti anayoipata kutoka kwa watu wake wa karibu akiwemo Mama yake mzazi
na wengine kibao.
Hapa chini ni mkataba ambao amelamba kutoka kampuni ya Emilates Hall kupiga shoo huko pande za Mtwara


No comments:
Post a Comment