Masombo
Lino kulia, baada ya kumpokonya mpira Kiggi kama alimuazima, akitaka
kugeuka kusukuma mashambulizi, Uwanja wa TCC jana. Jamaa ni mzuri kwa
kweli na Simba watamsahau Yondan.
BEKI wa Simba SC,
Masombo Lino Masombo Lino kutoka Daring Club Motema Pembe kutoka ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), jana alikuwa kivutio kikubwa
katika mazoezi ya klabu hiyo, Uwanja wa TCC, Chang’ombe, Dar es Salaam.
Katika mazoezi yaliyoongozwa na Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Mserbia
Milovan Cirkovick, Masombo alionyesha ni mzuri kwenye kuzuia na kusaidia
mashambulizi pia.
Mashabiki wa Simba walikuwa wenye furaha kubwa TCC jana kutokana na
mavituuz yaliyokuwa yakifanywa na wachezaji wao wengine wapya pia.
Mazoezi ya Simba yanaendelea leo kwenye Uwanja huo, kujiandaa na Klabu
Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, michuano iliyopangwa
kuanza Julai 14 hadi 29, mwakani.
Beki hilo la kati ambalo lilipiga soka ya uhakika mwaka jana wakati
Simba ilipokutana na DC Motema Pembe katika mechi ya mchujo kuwania
kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika lilitua jana Dar
es Salaam na leo imeelezwa limesaini mkataba.
Simba, mabingwa wa Ligi Kuu ya Bara, wamemsajili beki huyo kuziba pengo
la beki wao hodari, Kelvin Patrick Yondan ambaye amehamia kwa wapinzani,
Yanga.
No comments:
Post a Comment