Nyota
ya jaa ya mshambuliaji wa kimataifa wa Simba na Uganda Emmanuel Okwi,
inazidi kuwaka, siku chache baada ya klabu bingwa ya Orlando Pirates
kutuma barua ya kutaka mshambuliaji huyo wa Simba aende kufanya
majaribio kwenye klabu hiyo, leo hii timu pinzani ya Orlando kwenye ligi
ya Afrika kusini, Mamelodi Sundowns wameuambia uongozi wa Simba kwamba
wapo tayari kumnunua mshambuliaji huyo.
Taarifa
zilizothibitishwa kutoka ndani ya uongozi wa Simba zinasema kwamba
Mamelodi wametuma maombi ya kutaka kumsaini Okwi ambaye amekuwa na msimu
mzuri sana ndani na nje ya ligi kuu ya Vodacom msimu ulioisha.
Pia
chanzo changu hicho cha habari kutoka ndani ya Simba kilisema kwamba
kuna timu moja inayoshiriki ligi kuu ya Italia Serie A, wameonyesha nia
ya kumtaka Okwi lakini wamesema kwamba wanasubiri mpaka michuano ya Euro
itakapoisha ndipo watakapoamua juu ya suala la usajili wa mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa Uganda.

No comments:
Post a Comment