Staa wa filamu nchini
Tanzania, Aunty Ezekiel hayupo nchini kwa muda mrefu sasa na habari zinasema
amepiga kambi Dubai, huko.
Uarabuni ambako
anaendesha maisha yake ya kila siku.Kutoweka kwa msanii
huyo kulijulikana wiki iliyopita kwenye uzinduzi wa filamu ya Wema Sepetu ya
Super Star pale Hyatt Kilimanjaro Kempinsk Hotel, Dar es Salaam ambapo wadau
wengi walihoji aliko msanii huyo kutokana na tabia yake ya kutokosa
shughuli.
Baadhi ya marafiki zake
walisema yuko Dubai akiendesha maisha yake baada ya kuchoka na skendo za
Bongo.
“Mnamuulizamuuliza
Aunty, hamjui yupo Dubai, amechoka na maskendo ya Bongo, sasa anakula raha tu,”
alisema shoga yake mmoja ambaye si maarufu, lakini hakauki kwenye viwanja vya
kujirusha.
Habari nyingine
zinasema Aunty atarejea nchini wiki mbili zijazo lakini hatakaa sana atarudi
tena Dubai kuendelea na maisha yake ambayo si ya kucheza filamu tena kama
ilivyokuwa hapa Tanzania.

No comments:
Post a Comment