Wastara Juma.
Maombi ya watanzania pamoja na
michango yao ya fedha vimesaidia kumfikisha mwigizaji Sajuki hapa alipo
baada ya kupata nafuu kubwa toka apelekwe India kuitibiwa.
Wastara amesema Sajuki anaweza kuanza kuigiza hata sasa kwa sababu nguvu imesharudi,
anaweza kutembea kwa muda mrefu na hata hali yake ya sasa imebadilika sana tofauti na mwanzo.
Amesema “baada ya miezi mitatu Sajuki anaweza kuanza kuigiza kama yeye mwenyewe atapenda na hata sasa hivi alipo pale unaweza kwenda nae location hana wasiwasi wowote ila kwa sababu ni mtu amefanyiwa upasuaji anahitaji kupumzika zaidi huwezi kutoka nae kwa sababu kuigiza inahitaji akili zaidi lakini baada ya miezi mitatu au minne anaweza kuendelea na kazi zake kama kawaida”
kwenye sentensi nyingine Wastara amesema hawezi kuzuia Sajuki kupigwa picha za Tv na magazeti kwa sababu kupitia vyombo hivyo vya habari ndio walifahamu kwamba anaumwa na wakaamua kumchangia sasa ni lazima wajue pia anaendeleaje kupitia vyombo hivyo.

No comments:
Post a Comment