Mwandishi wa habari Albert G
Sengo kutoka Mwanza ameripoti kwamba majina ya watu watano
wanaotuhumiwa kuhusika moja kwa moja na kifo cha aliyekuwa Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mwanza Leberatus Barlow yametajwa na Polisi.
Akitaja hayo majina mbele ya
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema, Mkurugenzi wa upelelezi
wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba amesema simu iliyoporwa ya
mwanamama ambaye alikuwa akisindikizwa nyumbani na marehemu ndiyo
imesaidia kukamilisha upelelezi huo na wahusika kukamatwa.
Waliotajwa kuhusika na hayo mauaji
ni Muganyizi Michael Peter (36) ambaye ametajwa kwamba ndiye aliyemuua
Barlow, Chacha Waitare Mwita (50), Magige Mwita Marwa (48), Buganzi
Edward Kusuta pamoja na Bhoke Marwa Mwita (42) ambao wote wamekatwa
wakiwa Dar es Saalam walipokimbilia baada ya mauaji.
Alisema Kikosi kazi cha
upelelezi kilichokuwa chini yake Manumba kilijigawa kwenye makundi
matatu moja ni lile la Ukamataji, Mahojiano na jingine la intelijensia
huku wakitumia njia ya sanyansi kufatilia kupitia mitandao ya simu.
Kukamatwa kwa watuhumiwa hao
wa Dar na wale wa Mwanza kunafanya jumla yao kuwa 10 na bado jeshi
linasaka wengine Lakini chanzo cha hao wauaji kufanya hivyo bado
hakijatajwa.
Liberatus Barlow aliuawa Oktoba
13 mwaka huu, saa 8 usiku kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana
katika eneo la Minazi mitatu huko Kitangiri wakati alipopita
kumsindikiza Mwalimu Dorothy Moses nyumbani kwake kutoka katika kikao
cha harusi kilichofanyika Mtaa wa Rufiji.
No comments:
Post a Comment